Sasa wakati umefika wa kushika nilichonacho (mimi)
Kwa wema niende kwa Mungu nitoe zawadi
Sasa wakati umefika kwenda mbele ya Mungu wangu
(Ili) Aone nilivyoandaa zawadi ya leo
Nitamwambia Bwana pokea hiki kidogo nilichonacho
Kwani Mungu wewe wanijua mimi siwezi hata kueleza
Nakusihi sana Baba unipokee
Nigawie na baraka niwe salama
Mema yote niliyokuwa nayo yametoka kwa Mungu
Hivyo nami ni kosa kusahau kumshukuru
Kwani kuwepo hapa leo hii ni kazi ya nani
Kamwe mimi sitapata uwezo pasipo Mungu
Mema aliyotenda Mungu nijibu lini na vipi
Mbona hofu yazidi kuwa ndani ya moyo wangu
Mbele ya Bwana Mungu wangu kufanya siri ni bure
Yeye ndiye mpanga mambo yote ya wanadamu
Pumzi anayonipa uhai unatoka kwa nani
Bila Mungu hakika mwanadamu siwezi kitu
Nimepata nafasi hii leo ya kwenda kutoa zawadi
Heri niende ya kesho sio yangu ajua Mungu